Marekani imesema kuwa inapinga suala la Rais Paul Kagame wa Rwanda kugombea tena urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.
Shirika la Habari la Ufaransa AFP limeripoti kutoka Washington kwamba, baada ya bunge la Rwanda kutangaza kuwa litaifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ili imruhusu Rais Kagame aendelee kuongoza nchi hiyo, Marekani imetangaza kwa mara nyingine kuwa inapinga suala hilo.
Kipindi cha urais wa Paul Kagame kinamalizika mwaka 2017 nchini Rwanda.Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeelezea wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa bunge la Rwanda na rais wa nchi hiyo wa kuunda kamati maalumu ya kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ili iweze kumruhusu Kagame agombee tena urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment