Jeshi la polisi wilayani Iramba mkoani Singida limetumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kuwakamata mwenyekiti wa uhamashishaji kanda ya kati Bi Jesca Kishoa na katibu wa Bavita wilayani Iramba Bwana Reimani Minja, wakati walipokuwa wakiwahamasisha wananchi kwenye mkutano wa hadhara kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Akiongea kwa simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Bwana Thobias Sedoyeka amesema wao wanatekeleza amri ya mkuu wa wilaya ya Iramba ya kupiga marufuku na kuzuia mikutano yoyote ya hadhara ifanyike wilayan
Akieleza baada ya kuachiwa na jeshi la polisi alipokuwa amewekwa chini ya usalama kwa zaidi ya masaa matano, mwenyekiti wa uhamashishaji Chadema kanda ya kati Bi. Jesca Kishoa, amesema anashangaa kuona mkuu wa wilaya ya Iramba akiwakataza kufanya mikutano huku vyama vingine vimekuwa vikifanya mikutano, jambo ambalo hastahili kufanya hivyo kwa sababu yeye anatawala wananchi wenye vyama tofauti na siyo chama kimoja.
Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Iramba wametupia lawama kwa jeshi la polisi kuzuiA mikutano minne ya Chadema, pia kutumia nguvu kutawanya watu kwa kuwamwagia maji ya kuwasha na kuwapiga mbomu ya machozi.
No comments:
Post a Comment