Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo. Aidha, baada ya utenguzi huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifafanua moja ya swali lililoulizwa kutoka kwa mmoja Waandishi wa habari (hayupo pichani) kuhusiana na suala zima la kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa NIDA,katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mapema leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.Picha Michuzi Jr-MMG
RAIS Dk.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Dickson Mwaimu kwa ajili kupisha uchunguzi wa sh. Bilioni 179.6 zilizotolewa kwa ajili ya vitambulisho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi Ombeni Sefue amesema kutengua uteuzi huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji wa vitambulisho vya taifa kusimamishwa kazi ambao ni Mkurugenzi wa Tehama ,Joseph Makani , Afisa Ugamvi Mkuu, Rahel Mapande ,Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni ,pamoja na Afisa Usafirishaji ,George Ntalima.
Balozi Sefue,amesema kuwa kutengua uteuzi huo unatokana na kuwepo kwa malalamiko ambayo yamemfikia Rais juu ya wananchi kukosa vitambulisho vya taifa huku kukiwa na fedha ya Sh.Bilioni 179.6 zikiwa zimetumika .
Rais Dkt Magufuli ameitaka Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) ifanye uchunguzi kama kuna vitendo vya rushwa vimefanywa ,amezitaka taasi ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Mamlaka ya Manunuzi (PPRA) kufanya uchunguzi wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.
Amesema katika uchunguzi huo CAG ifanye uchunguzi na kuangalia vitambulisho vya taifa kama vinaendana na fedha iliyotumika ya sh.bilioni 179.6 .
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment