Katika hali ambayo imeonyesha kuwafurahisha wakazi wa kata ya Mnyanjani, mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Suleiman Khafidh amesema iwapo watamchagua atanunua helkopita kwa ajili ya kubebea wajawazito na wazee kuwapeleka hospitali.
Alizungumza hivi karibuni katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Mnyanjani, Khafidh alisisitiza wajawazito na wazee wanapata kero kubwa sana kufikia huduma za afya ambapo baadhi yao wanajifungulia njiani kutokana na ubovu wa barabara hivyo wakimchangua yeye tatizo hilo litakuwa historia, Atanunua helkopita . Kauli hiyo ilionekana kuwafurahisha sana wananchi ambao walimshangilia hivyo wakimtaka aitekeleze haraka.’’ Ndugu zangu mimi ndiye mgombea mdogo kuliko wote nitatekeleza” alisema Suleiman
No comments:
Post a Comment