What's Trending?

Labels

Ads

Friday, July 31, 2015

Pluijm apangua kikosi Yanga

BAADA ya kutolewa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu Kombe la Kagame, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amefumua kikosi chake.
Yanga walitolewa kwa mikwaju ya penalti 5-3 na Azam FC katika mchezo wa robo fainali uliochezwa Julai 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na Yanga kushiriki michuano hiyo lakini inaonekana Pluijm hajapata kikosi cha kwanza cha kudumu kutokana na kupangua kila wakati kikosi hicho.
Pluijm alionekana wazi kuanza kupangua kikosi chake katika mchezo wa robo fainali na mabadiliko aliyoyafanya kwenye kikosi chake yameonyesha wazi kwamba hadi sasa hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kupata namba katika kikosi chake.
Yanga waliosajili makipa watatu katika michuano hiyo walikuwa wakiwabadilisha kila mchezo Deogratias Munish ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’ hali inayonyesha kwamba, Pluijm bado hajapata kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment