Dimitri Payet akiachia shuti lililoipa Ufaransa ushindi wa 2-1 Ufaransa dhidi ya Romania. Picha na Getty
Goli lililofungwa na kiungo wa Ufaransa Dimitri Payet anayechezea timu ya West Ham katika Ligi Kuu ya Uingereza katika dakika ya 89 lilikuwa goli muhimu ambalo liliwafanya wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa fungua dimba wa michuano ya UEFA Euro 2016 kutoka Kundi A.
Kwa ujumla mchezo huo wa ufunguzi uliofanyikia katika Uwanja wa Stade de France, ulikuwa wa vuta nikuvute huku wenyeji Ufaransa wakionekana kuelemewa mara kwa mara. Mpaka timu zilipokwenda mapumziko ubao wa matangazo ulikuwa ukisoma 0-0.
Payet akishangilia goli lililowapa wenyeji Ufaransa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Romania.Picha na Getty Images.
Kunako dakika ya 58 ya mchezo, Olivier Giroud aliipatia Ufaransa bao la kuongoza. Hata hivyo Romania, kupitia Bogdan Stancu walifanikiwa kupata goli la kusawazisha kwa njia ya penati katika dakika ya 65 ya mchezo.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment