Baada ya kutangazwa kuwa ndiye atapeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao,Mheshimiwa John Magufuli akazungumza kisha kumteua mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu ujao
"Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kunifanya niwe salama...Nimehewa nafasi mliyonipa ni kubwa sana....Jana wakati naomba kura niliwaambia nitumeni nami nitawatumikia...nitawatumikia kwa nguvu zangu zote,kwa moyo wangu wote kwa kutumia vipaji vyangu vyote nilivyopewa na mwenyezi mungu...wingi wa kura hizi nilizopata ni uthibitisho kuwa CCM ni wamoja...naamini tutashirikiana ili kuutafsri ushindi huu katika uchaguzi mkuu ujao"- Dkt Magufuli."Kinachotakiwa ni ushirikiano kwa wanachama,wote,tuungane kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa chama chetu kinapata ushindi ulio mnono sana kwenye uchaguzi mkuu ujao...Nafurahi kuwa napeperusha chama imara,chenye watu wenye..hamasa ya juu,chama kilichoipatia sifa nzuri nchi yetu,chama kilicho komaa"- Dkt Magufuli.
"Waheshimiwa wanachama wenzangu wa CCM naomba kuwahakikishia kuwa nitakuwa nanyi kweli kweli,nitakuwa mtumishi wenu...hapa ni Chama Kwanza"- Magufuli.
"Nimekaa na kufikiria..imeamua kumteua mgombea mwenza wangu awe Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Baada ya kusema haya naomba tushirikiane ili CCM ipate ushindi,asanteni sana!!"- Magufuli
No comments:
Post a Comment