Mtiti! Prezidaa wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ ametembeza kichapo mtaani kwa kuwatandika bakora vijana waliokuwa wakimrekodi kwenye simu wakati akihangaika kufungua tairi la gari lake lililopata pancha.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilijiri hivi karibuni, maeneo ya Makumbusho, Dar, anakoishi staa huyo.
Awali, mwanamuziki huyo aliegesha gari lake hilo aina ya Toyota Mark X kwenye nyumba moja maeneo hayo ambapo alielekea nyumbani kwake, aliporudi alikuta tairi moja la mbele la upande wa kushoto limekwisha upepo (pacha) ndipo alipoanza kulifungua ili akalizibe kwa kuwa hakuwa na la ‘spea’.
Wakati akifanya zoezi hilo huku jua kali la jiji likiwaka na kumfanya atokwe na jasho jingi, aliwashtukia vijana ambao walikuwa wamekaa kwenye kibaraza cha nyumba nyingine ambao walikuwa wakimrekodi wakati akihangaika na gari lake.
Mara baada ya kumaliza shughuli ya ya kulifungua tairi hilo, akionekana kuchoka, jamaa huyo aliwasikia vijana hao wakimcheka ndipo akawafuata kwa hasira na kuwakunja kisha kuwanyang’anya simu waliyokuwa wakitumia kumrekodi.
Ishu hiyo ilizua songombingo ‘hevi’ huku watu wakimshangaa Chaz alivyokomaa akitaka kuipeleka simu hiyo polisi, jambo ambalo ‘madogo’ hao hawakuliafiki.
Hata hivyo, vijana hao waliposikia neno polisi na kweli walikuwa wamemrekodi, waliingiwa na woga, wakamwangukia Chaz ambaye aliwatandika bakora ndipo akawasamehe na kufuta video hiyo kwenye simu.
No comments:
Post a Comment