Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho bado anaendelea kulipiga danadana ombi la Arsenal wanaotaka kumsajili golikipa mkongwe wa Chelsea Petr Cech kwa dau la paundi milioni 11.
Washika bunduki wa London wanahitaji dili hilo likamilike wiki hii, lakini wanakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Mourinho.
Cech anataka kutua Emirates na inafahamika kwamba mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich hana mpango wa kumbakiza kipa huyo mwenye umri wa miaka 33.
Hata hivyo, Mourinho hataki kuwaimarisha wapinzani wake Arsenal kwa kumruhusu Cech kutua Arsenal.
Bosi huyo wa Chelsea ameomba Arsenal impatie Alex Oxlade-Chamberlain au Theo Walcott ili awape Cech, lakini Arsene Wenger amekataa mapendekezo hayo.
Mourinho anapenda kuona Cech anajiunga na Paris Saint Germain (PSG), ambao pia wanavutiwa na huduma yake.
No comments:
Post a Comment