What's Trending?

Labels

Ads

Wednesday, June 17, 2015

Afrika Kusini yatakiwa ijieleze kwa kumruhusu al Bashir

Mahakama moja nchini Afrika Kusini imeipatia serikali ya nchi hiyo muda wa siku saba kutoa maelezo kwa nini ilikaidi agizo la kumzuia Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan kuondoka nchini humo. 



Ndege ya Rais wa Sudan iliondoka Afrika Kusini juzi na kuelekea Khartoum siku moja tu baada ya Mahakama Kuu ya Pretoria kuamuru kuwa Afrika Kusini imzuie Rais wa Sudan kuondoka nchini humo. 



Itakumbukwa kuwa marufuku ya muda ilitolewa baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kutaka Rais wa Sudan akamatwe kwa tuhuma za kuhusiaka na jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika jimbo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo. Tuhuma ambazo zimekanushwa na Rais al Bashir. 



Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan aliwasili Afrika Kusini tarehe 12 mwezi huu kwa minajili ya kushiriki kwenye mkutano wa 25 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. 



Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa anaichukulia waranti ya kukamatwa Rais wa Sudan kama kadhia yenye uzito wa hali ya juu na kwamba mamlaka ya ICC yanapasa kuheshimiwa.

No comments:

Post a Comment