What's Trending?

Labels

Ads

Sunday, January 10, 2016

MABULA ASIKITISHWA NA UKOSEFU WA MAJI MWANZA,

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula akifafanua jambo ofisini kwake.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza (CCM) Stanslaus Mabula amesikitishwa na baadhi ya wakazi wa jimbo hilo kukabiliwa na ukosefu wa Maji safi na salama huku baadhi ya miradi ya maji ikichukua muda mrefu bila utekelezaji wake kukamilika kwa wakati.
Mabula ameelezea masikitiko yake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa jimbo la Nyamagana, juu ya kukosa huduma ya maji ya bomba licha ya jimbo hili kuzungukwa na ziwa Victoria.
Mabula ambae alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza katika uongozi uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana, amebainisha kuwa ipo miradi ya maji ambayo bado haijatekelezwa kutokana na serikali kushindwa kutoa pesa kwa wakati jambo ambalo amesema kuwa atalisemea mara kwa mara katika vikao vya bunge lijalo ili kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Bonyeza PLAY Hapa Chini Kusikiliza
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

No comments:

Post a Comment