Na Hillary kasambala: 0712444114.
Nyuma ya Mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke. Je nyuma ya mwanamke aliyefanikiwa kuna nani? Unaweza ukawa haujawahi kujiuliza swali kama hili na inawezekana baada ya kulisoma swali hili katika makala yangu usipate majibu ya kina na yenye tija ndio maana leo najadili swala hili kwa jicho la saikolojia.Licha ya tafiti nyingi
kufanywa na mashirika ya ndani na nje ya nchi likiwepo “UNICEF’’ tafiti ya mwisho kufanywa 2009, ilionyesha kwamba takribania wasichana 3 kati ya 10 wameripi walau tukio moja la ukatili wa kijinsia kabla ya umri wa miaka 18. Swali Je Kwa nini sasa ukatili wa kijinsia unaonekana umekithiri kuliko nyakati za nyuma?Karne za huko nyuma ukatili wa kijinsia haukuwepo? Majibu ya maswali haya ni mafupi,lazima tukubali kwamba ukatili wa kijinsia ulikuwepo kwa miaka mingi kizazi hadi kizazi ila tulikuwa hatujapiga hatua ya kitekinologia, hapa namaanisha ujio wa utandawazi uliunganisha dunia kama kijiji na kufanya taarifa kusafiri kwa haraka na vyote vilirahisishwa kupitia tv,radio,computer,enternet,I pad na simu za viganjani kama smartphone,tabulate pamoja na mitandao ya kijamii kama facebook,twitter,whatsup ,Skype na instagram ambapo mtumiaji anaweza kuona tukio, kupiga picha na papo hapo kutuma kwenye mtandao vyote hivi vikisaidiwa na satellite zinazozunguka juu ya anga. Ukatili wa kijinsia ni janga lililojengwa kwa misingi ya kihistoria na tamaduni zilitumika kupiga chapa katika akili za wanaume na jamii kwa ujumla, hivyo kutumia sheria na kanuni pekee kutatua migogoro kuhusu janga hili kwa kuwaadhibu wanaotenda unyama huu pekee haitosha kutatua tatizo, Ndio maana naona uhitaji wa saikolojia kuhusika kwa sababu ndio kitu pekee kitumiacho sayansi kuweza kumwelewa na kutambua akili na tabia za watu.
Ndugu msomaji wangu leo najadili namna jamii na tamaduni zilivyoweza kupanda nguvu ya ziada nyuma ya mwanaume bila kutegemea kwamba nguvu hizo zingetengeneza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake kwa maana ukatili huu haukupangwa bali ulikuja kama changamoto,hivyo jamii na tamaduni zilitengeneza misingi mikuu miwili nayo ni:-
Kummilikisha Mali, Mwanaume alipewa uwezo wa kumiliki mali kama kiongozi , lazima tukubali kwamba kwenye kila kikundi lazima kuwe na kiongozi hata wanyama na wadudu wanaviongozi, jamii na tamaduni ilimpa Mwanaume nafasi ya kumiliki ardhi na Rasilimali kwa maana nzuri nayo ni kumfanya awe mtu anayeweza kuonyesha njia,dira na kuzisimamia lakini Mwishowe dhana hii ikaathiri akili za wanaume na ikatengeneza uhusiano usio sawa baina ya mwanamke na mwanaume na hatimaye mwanamke akanza kudhalilishawa na kunyanyaswa na mwishowe akafanywa kuwa kiumbe dhaifu, mwoga na asiyeweza kujitegemea mwenyewe kuthibitisha hili,Joseph Schumpeter 1883 aliyesomea sayansi ya siasa katika chuo cha Havard University na kutunukiwa nishani ya uprofessor “anasema kwa asili mwanadamu ameumba na hulka ya kupenda kutawala mwingine hivyo ukitaka kumtawala mtu sharti la kwanza ni kushika na kumiliki uchumi wake”.
Itaendelea…….

Imeandaliwa na Hillary Kasambala 0712444114

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment