List ya mastaa wa Bongo Tanzania ambao walijitosa na kujipanga kwenye foleni ya kuusaka Ubunge iliongezeka baada ya mchekeshaji kutoka Kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji nae kujitosa kwenye foleni hiyo.
Masanja alithibitisha kwamba kazi ya Ubunge anaiweza “Orijino Komedi ipo, mimi sio member wa kundi, mimi ni mwanzilishi.. siwezi kuacha Komedi, mbona nilikuwa Mchungaji na sikuacha Komedi.. nitakuwa Mbunge, Komedi na Church…” Hii ni siku chache zilizopita kwenye exclusive interview na millardayo.com pamoja na Amplifaya.
Kura hazikutosha kwake, maana yake ni kwamba kwenye Kura za maoni upande wa makada wa CCM Ludewa, Masanja hajafanikiwa kupita… lakini aliahidi pia hata kama akishindwa bado ataendela kumpa support yule atakaepita.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Masanja ameandika haya kukubali matokeo “Ludewa ….. Dah! Najipanga nitarudi tena. Sasa ni muda wa kumpigia kampeni aliyepita ili akatuwakilishe Bungeni. HapaKaziTu” @mkandamizaji
Kwenye ukurasa wake instagram ameandika
Jamani uchaguzi wa kura za maoni umeisha.
nimepata kura jumla kwa zoooote ukihesabu nimebeba jumla kabisa kabisa kura ukijulisha vizuri kabisaaa utulie nimepata kura hiziiiiƬ 19
No comments:
Post a Comment