What's Trending?

Labels

Ads

Sunday, November 15, 2015

KAMATI KUU YA CCM YAPITISHA MAJINA MATATU YA WAGOMBEA USPIKA,SITTA NCHIMBI CHALI

post-feature-image Majina hayo yamepenya kutoka katika orodha ya majina 21, miongoni mwao akiwemo Spika wa Bunge la 9, Samuel Sitta, Dkt. Didas Masaburi ambaye alitangaza kujitoa katika dakika za mwisho, Dkt Kalokola na wengineo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni ya leo baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichoongozwa na mwenyekiti wake Dkt Jakaya Kikwete mjini Dodoma, jina moja kati ya hayo matatu litatangazwa kesho Jumatatu ikiwa ni pamoja na jina la mgombea wa nafasi ya Naibu Spika.
Katika waliopitishwa:
Job Ndugai ni mbunge mteule jimbo la Kongwa Dodoma na pia alikuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita.
Dkt Tulia Ackson ni Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali, pia alikuwa ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akitokea taasisi za elimu ya juu. Amekuwa mhadhiri wa sheria katika kitivo (sasa shule) cha sheria chuo kikuu cha Dar es salaam.
Abdullah Mwinyi ni mtoto wa Rais mstaafu Al Hajj Aly Hassan Mwinyi na ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.


Wana-CCM hao watatu watapigiwa kura na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma ilikuchagua jina moja kugombea nafasi hiyo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kuhusu nafasi ya Naibu Spika, alisema kulikuwa na kasoro za kutofuata kanuni za chama ambapo hadi jana ni mwanachama mmoja tu ndiye aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu,’ lakini atatakiwa kuchukua fomu upya.

“Ibara ya 57, Kanuni za kamati ya wabunge wote wa CCM toleo la 2010 toleo la nne 2011, mbunge yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Naibu Spika atatakiwa kuchukua fomu kupitia kamati hiyo na atairudisha kisha kamati itakaa kupata jina moja,” alisema Nape.

Kwa mujibu wa maelezo hayo mbunge wa chama hicho anayetaka kugombea Unaibu Spika, atatakiwa kuchukua fomu leo Novemba 16, kwa ada ya Sh 100,000 kisha atairudisha kesho Novemba 17, ndipo kamati itakaa kuchambua na kupitisha jina moja.
Je, Nani kati ya hawa watatu apewe nafasi na CCM?

        
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

No comments:

Post a Comment