What's Trending?

Labels

Ads

Friday, November 13, 2015

ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MORO MJINI ASAKWA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI KWA KUMTWANGA MAKONDE KATIBU MWENEZI CHADEMA.

 Aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Morogoro mjini , kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Albanie Marcossy hapo katika picha juu anatafutwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa madai ya kumshambulia kwa kumpiga Katibu mwenezi wa chama hicho wilaya Shabani Dimoso katika ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa Ngoto.
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Leonald Paulo akizungumza na waandishi wahabari jana alisema kuwa Marcossy anadaiwa kufanya tukio hilo mwishoni mwa wiki.

Paulo alisema mtuhumiwa Marcossy alifanya tukio hilo baada ya kumkuta katibu huyo Mwenezi kwenye ofisi za chama hicho zilizopo katika mtaa wa Ngoto Manispaa ya Morogoro na baadae kuondoka.

Baadhi ya mashuhuda tukio hilo ambao hawakuta majina yao kuandikwa walisema kuwa mgombea huyo alipofika katika ofisi hizo alianza kumshambulia katibu huyo kwa maneno kuwa anamtangazia kwa wananchi kuwa amekula fedha za mawakala wa kusimamia uchaguzi na ndipo alipoanza kumshambulia kwa kumpiga wakiwa ndani ya ofisi hiyo.

Mashuhuda huo walisema kuwa wakati tukio hilo linatokea katika ofisi hizo ndani kuliwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na kuamulia ugomvi na kisha kumuondoa mgombea huyo katika eneo hilo la ofisi.

Alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo Katibu huyo mwenezi wa Chadema Shabani Dimoso alikiri kushambuliwa kwa kupigwa na mgombea huyo akimtuhumu mambo mbalimbali ikiwemo ya madai ya kumtangazia kuwa amekula fedha za mawakala kitu ambacho alidai si cha kweli.

Dimoso alisema kutokana na shambulio hilo pamoja na kupewa vitisho na mgombea huyo alilazimika kwenda kufungua kesi katika kituo kikuu cha Polisi Morogoro huku suala hilo pia likishugulikiwa na viongozi wa juu wa Chadema.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwansidhi wa habari hizi Marcossyalisema kwa sasa hawezi kusema lolote kuhusiana na tuhuma hizo kwa kuwa hajapata taarifa zozote kutoka jeshi la polisi kama anatafutwa dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

“Mimi nipo na hakuna barua yoyote wala taarifa kutoka jeshi la polisi niliyopata kama natafutwa hivyo nasubiri hilo na nitawajuza”alisema Marcossy ambaye hakutaja sehemu ya moja kwa moja alipo

Katika sakata la madai ya mawakala waliokuwa wanasimamia uchaguzi mkuuu wanadia malipo yao,alisema hajui lolote kuhusu sakata hilo na mawakala hao wawaulize waliowatafuta ni nani kuliko kumtupia lawama yeye.

Aidha alisema mawakala hao kipindi wanatafutwa walipewa maelezo ni nani atayehusika na kuwalipa fedha zao hivyo ana shangaa mawakala hao kusema kwamba kakimbia na fedha zao jambo ambalo halina ukweli wowote ndani yake.

Katibu mkuu wa Chadema mkoa wa Morogoro Samuel Kitwika alipoulizwa kama amepokea taarifa ya kushambuliwa kwa katibu mwenezi na mgombea huyo alisema hajui lolote na kwamba hajapokea malalamiko yoyote mpaka sasa.

Kitwika alisema kwa ujumla chama kiko shwari na hakuna migogoro yoyote na kama atafikishiwa malalamiko hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

No comments:

Post a Comment