What's Trending?

Labels

Ads

Thursday, August 6, 2015

BREAKING NEWS: IBRAHIMU LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI CUF

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Rasmu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya
wananchi (UKAWA)  katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Profesa Ibrahimu Lipumba amesema amechukua uamuzi huo kutokana na Ukawa kushindwa kusimamia makubaliano waliyokunaliana na sasa atabaki kuwa mwanachama.
Vuguvugu za kujiuzulu kwake zilianza juzi katika mitandao ya kijamii baada ya mwenyekiti huyo kutoonekana kwenye mkutano mkuu wa UKAWA walipompitisha Edward Lowassa kupeperusha bendera ya UKAWA kwenye mbio za Urais 2015 na Juma Dudi Haji kama mgombea mwenza.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa  mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Iblahimu Lipumba akitanga kujihuzuru wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa

No comments:

Post a Comment