Banza Stone enzi za Uhai wake.
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Banza Stone amefariki dunia leo hii Ijumaa. Ramadhani Masanja amefikwa na umauti kutokana na kuandamwa muda mrefu na magonjwa
Banza Stone (wa kwanza kulia) akiwa na Bendi ya Muziki Ya Twanga Pepeta
Shabani Ally Masanja ambae ni kaka wa Banza amethibitisha kutokea kifo cha Banza Stone nyumbani Sinza na msiba uko Sinza njia panda ya Lion. Banza Stone alikuwa anaugua ugonjwa wa fungus ya kichwa na kifua.
Banza Stone aliyezaliwa mwaka 1972 na kufanikiwa kumaliza elimu ya msingi katika shule ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwaka 1987, alianza taratibu kujihusisha na masuala ya muziki akiwa angali mdogo.
Banza alianza muziki miaka 25 iliyopita, mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya msingi kwa kujihusisha na muziki wa Hip Hop, enzi hizo walikuwa wakisikiliza katika redio. Wakati huo alikuwa na wenzake kama kina K One na Scoz Man.
Wazazi wake waliweka pingamizi baada ya kuonekana muziki huo kuwa wa kihuni na mwaka 1990 akaamua kuanza mchakato mpya wa kuwa mcheza dansi, alicheza dansi kwenye maharusi na kufanikiwa kupata fedha kidogo. Banza aliamua kwenda shule kusomea masuala ya mziki kwenye chuo cha utamaduni cha Korea, Korea Cultural Music Centre mwaka 1990 mpaka 1991.
Baada ya kuhitimu cheti alianza kuimba katika bendi mbalimbali ikiwamo The Heart Strings, Twiga Band, Achigo Band kama mpiga ngoma, Afri-Swez na bendi nyingine ndogo ndogo. Alikuwa akidumu katika bendi kwa miezi kadhaa, kabla ya kuhamia katika bendi nyingine mpaka alipoingia katika bendi ya The African Stars, Twanga Pepeta na kuijenga bendi hiyo barabara.
Alijiunga na chuo cha Sanaa Bagamoyo mwaka 2000 ambapo alipata mafunzo kwa miaka miwili, alipomaliza alitoka Twanga Pepeta na kwenda Tanzania One Theatre (TOT) na huko alijulikana zaidi kwa jina la Mwalimu wa Walimu japo hakukaa sana na kuamua kuanzisha bendi yake iliyokuwa ikiitwa Bambino Sound ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa tu lakini ilivunjika kutokana na kutokuwa na uongozi mzuri na akarudi African stars Band na baadae kuhamia Extra Bongo.
Katika kipindi cha miaka 24 tangu aanze muziki wa dansi rasmi haikuwa rahisi kwake kupata mafanikio, kwani alizunguka sana mpaka kuifikia bendi ya The African Stars Twanga Pepeta mwaka 1995. Banza Stone alipitia zaidi ya bendi tisa ikiwemo Rufita Band. Mwaka juzi msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Ramadhani H-Baba aliamua kumshirikisha Banza kurekodi wimbo wake mpya wa Sina Raha.
Banza Stone amewahi kutamba na nyimbo kadhaa zikiwemo: Mtaji wa Maskini, Kumekucha, Elimu ya Mjinga, Angurumapo Simba Mcheza Nani na Falsafa ya Maisha. Amewahi pia kuimba vibao kadhaa vya taarabu ukiwamo Kuzaliwa Mjini na ule wa Play Boy.
What's Trending?
Labels
- abdu kiba
- africa
- ali kiba
- Audio Music
- baraka da prince
- Baraka Da Prince New songs
- Baraka Da Prince New Songs 2016
- barnabas
- Barnabas classic new songs 2016
- belle 9
- ben pol
- ben pol new songs
- bill nass
- Bownload Nyimbo Mpya za Bongflava 2016
- Bushoke
- Bushoke New Song
- Bushoke Songs
- Bwana Misosi
- ccm
- chadema
- chege
- Christina Shusho New Songs 2016
- Christina Shusho - Nangoja New Songs 2016
- dauna nyange
- Daynaa Nyange New Song
- diamond platnum
- dogo janja
- Download Yamoto Band New songs 2016
- download bill nas new songs
- Download Dully sykes songs
- Download Juma Nature Songs
- Download Meda Classic Songs
- DOWNLOAD NEW BONGOFLAVA 2016
- Download Nyimbo mpya ya Harmonize
- Download Nyimbo Mpya za Bongflava 2016
- Download Nyimbo za Neyba
- Download Nyimbo za Bushoke
- Download Tanzanian Music
- Downloda Nyimbo za WASAFI 2016
- Fid q New Song
- Gorko flow
- gospel songs
- habari za kimataifa
- habari za kitaifa
- habari za michezo na burudani
- habari za siasa
- harmonize
- Harmonize New Songs 2016
- historia mbalimbali
- izzo bisness Nyimbo mpya
- izzo busness
- javascript:void(0);
- jay dee
- Juliana Kanyomozi
- jux
- kala jeremaya
- kala jeremaya New Songs
- kimbunga
- Koffi Olomide
- linah
- lowasa
- madee
- madilu system
- MAGAZETI
- magazeti ya Tanzania
- magufuli
- mah
- matokeo
- matonya
- Matonya New Songs
- meda classic
- michezo
- movies
- mr blue
- MTIWADWA
- music video
- Mwana fA
- nay wa mitego
- NEW BONGOFLAVA 2016
- Ney wa Mitego nyimbo Mpya
- Neyba New Songs 2016
- Nyimb za Fid Q
- Nyimbo mpya
- nyimbo mpya za Bongoflava 2016
- Nyimbo mya za Shetta
- Nyimbo za shollo mwamba
- Nyimbo za Chege TMK
- nyimbo za dini
- nyimbo za injili
- Nyimbo za Madee
- nyimbo za man fongo
- Nyimbo za Matonya
- Nyimbo za Peter Msechu
- Nyimbo za Rama Dee
- Nyimbo za RAYMOND (Rayvan) Tiptop
- Nyimbo za Rich Mavoko
- Nyimbo za Shilole
- Nyimo za Mo Music
- Nyimo za MSAMI (Msami New song )
- Papa Wemba
- peter msechu
- Peter Msechu New Songs 2016
- quick rocka
- raymond
- recho
- rich mavoko
- roma
- shetta
- Shetta New Songs 2016
- Shetta Songs
- Shilole New Songs
- simba fc
- singeli
- Solomon Mukubwa New song 2016
- stamina
- tamaduni music
- technology
- The Best Song Of DARASSA
- The Best Song Of Diamon Platnums
- vichekesho
- video mbalimbali
- videos
- walter chillambo
- weusi
- yamoto band
- Yamoto Band New song
- yanga fc
- young dee
- young killer
Ads
Friday, July 17, 2015
michezo
Home
/
habari za kitaifa
/
michezo
/
TANZIA: Msanii wa muziki wa Dansi, Banza Stone(Ramadhani Masanja) afariki Dunia
TANZIA: Msanii wa muziki wa Dansi, Banza Stone(Ramadhani Masanja) afariki Dunia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment