Tangu wakati huo kumekuwa na tetesi kuwa alikuwa atangaze kujiondoa CCM.
Lowassa ni miongoni mwa makada 38 waliojitosa kuwania kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya urais wa CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Hata hivyo, jina lake halikuwamo katika orodha ya makada watano waliopitishwa kwenye vikao vya juu vya chama hicho ambavyo mwishowe vilimteua John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais atakayekabiliana na wagombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu huo. CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment