What's Trending?

Labels

Ads

Tuesday, July 7, 2015

Mhasibu TSN awania jimbo la Waziri Mkuu

MHASIBU  wa Kampuni ya Serikali (TSN)  inayochapia  magazeti ya Dailynews, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo Shafi Mpenda (36) ametangaza  rasmi  nia ya kugombea  ubunge  katika Jimbo la Mlele  mkoani Katavi kupitia CCM  katika uchanguzi  mkuu unaotarajiwa kufanyika  Oktoba 2015.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda  ambaye  anashikilia  Jimbo  hilo  la Mlele ameshatangaza rasmi  kuwa hatagombea  tena .

“Nikiwa mzawa wa jimbo hili, nilitafakari kwa makini sana, na kujiuliza maswali mengi sana……….

Hatimaye  nimepata majibu kwamba baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye taasisi yaSserikali, wakati  umefika wa kurudi nyumbani na  kuwa karibu zaidi na wananchi  wenzangu wa jimbo hili ili  niweze kuwatumikia na kutoa mchango wangu katika  maendeleo  ya jimbo letu na  mkoa wa Katavi kwa ujumla wake.

Nawaomba wananchi wenzangu waniamini  kwamba Kazi hii naiweza,  naimudu, nimejipima na nimeona natosha katika kuwa sauti kwa wale wasio na sauti ……….. Baada ya kuangalia changamoto tulizonazo, najua wapi  tunataka kwenda  ikizingatiwa kwamba Katavi  bado tupo nyuma sana kimaendeleo” alieleza .

Akifafanua anaongeza kuwa Mbunge wa Jimbo  hilo Pinda ambae pia ni Waziri Mkuu  amefanya mambo makubwa sana ya kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Katavi na  wilaya mpya ya Mlele.

“ Kwa maana nyingine ni kwamba, serikali sasa  imesogea karibu na wananchi kwa ajili ya kuwahudumia vizuri  zaidi……..

 Aidha, mzee Pinda ametoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya elimu, na sekta hii ni miongoni mwa mambo ambayo nakusudia kuyapa kipaumbele iwapo wana CCM wenzangu watanichagua kwenye kura ya maoni  na kunipa ridhaa ili niweze kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba, 2015” alibainisha

Alitaja meneo mengine ya kipaumbele kuwa  ni   pamoja na  kilimo ambacho kinajumuisha bei ya mazao ya biashara kwa mfano tumbaku,

“ Kero zinazowakabili watu wa katavi ni nyingi na zinahitaji mtu imara kama Mzee pinda mwenye uwezo mkubwa wa kubuni miradi mbalimbali itakayoweza kuharakisha maendeleo ya katavi. Miongoni mwa kero kubwa ni pamoja na migogoro kati ya wakulima na wafugaji, Mawasiliano ya simu, barabara na Reli, maji, afya pamoja na elimu”  alieleza

Aliongeza kuwa  nachokiona  yeye (Mpenda)   ni  fursa nyingi za kuleta mabadiliko  katika  mkoa wa Katavi  ambazo zinahitaji mtu makini, mbunifu, mwenye uwezo mkubwa wa  kushughulikia mabadiliko kwa kasi na kwa vitendo, aliye tayari kutumwa na akatumika, msikivu na mwenye hofu ya mungu, mwenye upendo na aliyekulia katika kupenda maendeleo.

Wengine ambao  wamejitokeza kutaka kurithi mikoba ya Waziri Mkuu  Pinda ni pamoja  Kamwele Isack Kilinda ambaye ni Meneja wa Tanroads mkoa wa Katavi,  Lephy Gembe ambaye ni  Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Emmanuel Nzumba ambaye ni Mfanyakazi wa Tanapa-Simiyu.

Kadhalika wengine ni pamoja na , Maganga Kampala ambaye ni  mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM, Richard Mbogo ambaye ni Kamanda wa Vijana CCM wilaya ya Mlele, Oscar Albano ambaye ni Mtaalamu wa kilimo, Pudenciana Kikwembe ambaye ni Mbunge wa viti maalumu jimbo la katavi.

No comments:

Post a Comment