
Mtoto wa mwimbaji maarufu wa zamani hayati Whitney Houston amefariki duniani Jumapili
Kristina Bobbi KBrown amefariki dunia baada ya kuugua kwa miezi saba . Taarifa zilizothibitishwa na vyombo vya vhabari kadhaa vya Marekani vinasema Christina alifariki Jumapili.
Binti Bobbi Kristina Brown ambae pia baba yake ni mwimbaji maarufu wa R&B Bobby Brown amefariki baada ya takriban miezi 7 tangu alipopatikana akiwa amezirai kwenye bafu na kukimbizwa hospitali .
Bobbi Christina mwenye umri wa miaka 22 alikutwa akiwa ameanguka ndani ya nyumba kwenye jimbo la Atlanta , Georgia alipokuwa akiishi na Nick Brown aliyemwita mumewe.
chanzo cha habari ni Sauti ya Amerika
No comments:
Post a Comment