Jonas Mkude tayari amerejea nchini Tanzania akitokea Afrika Kusini ambako alikwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits FC inayoshiriki ligi kuu (PSL) ya nchini humo.
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kwamba, kiungo huyo wa Simba ameshindwa kufaulu kwenye majaribio hayo.
Afisa habari wa klabu ya Simba Hajji Manara amesema bado hajapata taarifa yoyote ya kufaulu au kufeli kwa Mkude kwenye majaribio aliyokuwa akifanya kwenye klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini.
“Sijapata hiyo taarifa kiukweli, Jonas yupo na timu lakini sijapata taarifa kwamba mefeli au amefaulu kwasababu nikikuwa na pilika nyingi za ‘Ramadhani’ na sijasoma vyombo vya habari kwahiyo siwezi kusema lolote”, amesema Manara.
Timu (Simba) imeondoka juzi kuelekea Lushoto kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kwahiyo siwezi kujua ‘position’ yake mpaka leo nitakapokuwa ofisini ndipo ntaweza kulitolea tamko”, ameeleza.
source:
shaffihdauda.co.tz
source:
shaffihdauda.co.tz
No comments:
Post a Comment