What's Trending?

Labels

Ads

Wednesday, July 1, 2015

JAPAN YAITUPA NJE ENGLAD NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE

England women 1Timu ya taifa ya wanawake ya England imetupwa nje ya michuano ya kombe la dunia la wanawake kwenye mchezo wa nusu fainali kwa kichapo cha goli 2-1 kutoka  kwa Japan ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo kwenye
michuano inayoendelea huko nchini Canada.
England womenJapani walikuwa wakwanza kupata goli la kwanza dakika ya 33 kupitia kwa  nahodha wao Aya Miyama baada ya Claire Rafferty kumfanyia madhambi Saori Ariyoshi nje kidogo ya eneo la hatari lakini mwamuzi akaamuru ipigwe penati na Miyami akaukwamisha mpira kambani.
England women 2Dakika saba baadae, England walisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati pia kupitia kwa Fara Williams aliyefunga penati hiyo.
Goli la kujifunga la Laura Bassett dakika za majeruhi liliwapa ushindi Japan na kuwapeleka kwenye hatua ya fainali ambako watakutana na timu ya taifa ya Marekani.


No comments:

Post a Comment