
![]() |
| Waziri Prof Mwandosya akitafakari jambo |
![]() |
| Dereva wa gari alilokodi Prof Mwandosya Iringa na rubani wa ndege aliyokodi waziri huyo wakiagana |
![]() |
| Waziri Prof Mwandosya na mkewe akishuka katika gari la kukodi leo ofisi za CCM wilaya ya Iringa vijijini |
![]() |
| Waziri Prof Mwandosya akizungumza na wanahabari mkoa wa Iringa |
![]() |
| Mke wa waziri Prof Mwandosya ,katibu msaidizi wa CCM Iringa vijijini Bw Jackson na waziri Prof Mark Mwandosya wakisikiliza maswali ya wadhamini |
![]() |
| Baadhi ya wadhamini wa waziri Prof Mwandosya |
![]() |
| Katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Bw Hakim Jackson (kushoto) akimkabidhi Prof Mark Mwandosya fomu yenye majina ya wadhamini wake mkoani Iringa |
![]() |
| Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Iringa vijijini Shakra Kiwanga akimpongeza Prof Mwandosya |
![]() |
| Prof Mwandosya akiwaaga wadhamini wake |
![]() |
| Prof Mwandosya na mkewe wakiingia katika ndege tayari kwa safari ya kwenda mkoa wa Tabora na Kigoma |
Prof Mwadosya akifurahia kupata fomu ya wadhamini wake
>....................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
>....................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI asiye kuwa na wizara maalum Prof Mark Mwandosya ambae ni mmoja kati ya wana chama wa chama cha mapinduzi zaidi ya 35 walijitokeza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM amesema kuwa baada ya mwaka 2005 kushika nafasi ya tatu katika kinyang'anyiro cha Urais ni matumaini yake mwaka huu atafanya vizuri zaidi kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya wote waliojitokeza sasa.
"Wewe una mtoto anasoma darasa la tatu mfano na darasa kati ya watoto 90 yeye amekuwa wa tatu ukiwa kama mzazi lazima utampongeza na kumweleza kuwa uongeza jitihada na mtihani ujao baada ya kuongeza jitihada kuwa mwanangu nataka mtihani ujao uwe wa kwanza sawa anakujibu sawa ......sasa mimi mwaka 2005 nilikuwa wa tatu sasa unataka kuniambia nini tena"alihoji Prof Mwandosya huku wote wote pamoja na wanahabari wakiangua kicheko .
Akizungumza na wanahabari leo katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa vijijini mara baada ya kudhaminiwa na wanachama 28 wa CCM ,Prof Mwandosya alisema kuwa safari yake ni safari ya uhakika na hivyo iwapo chama chake kitamteua kuwa mgombea watanzania wategemee kuwa na nchi yenye uchumi bora .
Prof Mwandosya ambae aliulizwa na wanahabari hao kuwa anajambo gani jipya la kulifanya ambalo Rais anayemaliza muda wake Dr Jakaya Kikwete hakufanya alisema kuwa si kweli kama serikali ya Dr Kikwete haikufanya lolote japo alisema kiwa awamu ina changamoto zake na kila awamu imefanya mambo makubwa
"Kusema unalinganisha na serikali iliyopo ni kama vile unataka kusema serikali zilizotangulia hazikufanya lolote ama hazikufikia malengo yaliyotarajiwa ukweli ni vipindi katika uongozi wa nchi ambavyo vinatofautiana mfano miaka iliyopita mimi nikiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi simu hizi za mikononi ambazo matumizi yake ni makubwa hazikuwepo ila sasa kuna simu ambayo ni kamera ,Voice recoda na pia ni kopyuta hiyo hiyo sasa huwezi linganisha miaka hiyo na sasa na huwezi sema serikali iliyopita haikufanya ukweli kila serikali imefanya kulingana na wakati wake."
Alisema kuwa atafanya zaidi ya serikali iliyopita ama chini ya serikali iliyopita bado si jibu la kumsaidia mtanzania kwani alisema katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005 -2010 ujenzi wa chuo kikuu cha Dodoma haukuwepo na wala haikuwa ni ahadi ya Rais Dr Kikwete ila kutokana na kuna kuna haja ya kuanzisha chuo hicho serikali iliweza kuadhimia na kufanikiwa kuanzisha chuo hicho ambacho ndicho chuo bora nchini na Afrika Mashariki .
Hata hivyo alisema kuwa kwa kuwa kipaumbele chake kikubwa ni kujenga uchumi bora pia ana amini kupitia uchumi bora hakuna jambo litakaloshindikana kwani katika uchumi bora itakuwa ni vigumu kuzungumzia uchumi bora kama miundo mbinu haitaboreshwa wala bila kuwepo kwa kilimo na masoko ama kuwa na masoko bila viwanda au kuzungumzia kukuza uchumi bila kuwa na elimu bora .
Prof Mwandosya alisema kuwa mbali ya kuwa ni waziri ila bado anaishi na jamii na pia anatambua mazuri mengi yaliyofanywa na Rais Dr Kikwete na changamoto zake hivyo akiingia Ikulu lazima yale mazuri yote yaliyofanywa na serikali iliyopita atayaendeleza zaidi ya hapo yalipoachiwa na zile changamoto kuweza kuzitafutia majibu sahihi kwa faida ya jamii ya kitanzania.
Pia alisema mambo mengi anayatambua vema kwa kuwa yupo jikoni na mengine anayatambua vizuri kutoka kwa jamii ambayo imemlalamikia hivyo jukumu la kuyatekeleza lipo mikononi mwake na kuwataka wananchi hasa wana CCM kuendelea kujenga imani zaidi kwake .
" Lazima kuwa na vipaumbele ambavyo ni majibu ya mwananchi katika kukuza uchumi kwani huwezi chukua elimu ukaacha miundo mbinu kwani miundo mbinu ndio itakuza uchumi na huwezi zungumzia afya bila kuboresha elimu ....ukifanya haya makubwa manne hapo ndipo unageukia upande wa pili.....niseme tu kuwa uchumi unapokuwa lazima unazungumzia takwimu na kuona kipato cha Taifa kinaongezeka"
Waziri Prof Mwandosya alisema kuwa katika utawala wake kama Rais ni kuona anakuza uchumi zaidi kupitia kilimo huku akiamini kuwa asilimia zaidi ya 80 ya watanzania wanategemea zaidi kilimo katika kuendesha maisha yao na kilimo pia kinaweza kukuza uchumi haraka zaidi .
Katika hatua nyingine Prof Mwandosya amewataka wagombea wenzake kuheshimu taratibu za CCM katika mchakato wa kutafuta wadhamini badala ya kugeuza mbio hizo kama sehemu ya kuonyesha umarufu usio na tija na kuwa utaratibu wa CCM ni kupata wadhamini 450 pekee pasipo mbwembwe za aina yoyote pia vigezo vya mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania vipo wazi kuanzia kiwango chake cha elimu na awe na miaka kuanzia 40 kuwataka wote watia nia kujitathimini badala ya kuingiza mchezo katika suala hilo nyeti.
Prof Mwandosya aliwataka wagombea wenzake ndani ya CCM wasilalamike kwa kukumbushwa ukweli na madudu waliyoyafanya wakati wakiwa serikalini kwani ni vigumu watanzania kusahau maovu ya mgombea yeyote na kuwa anachojivunia yeye katika uongozi wake toka kipindi cha hayati baba wa Taifa hadi sasa hajapata kuwa na sifa mbaya kama baadhi ya wagombea wengine ambao wamechukua fomu ya kuomba kuaminiwa na CCM mbali ya kuwa na sifa mbaya kwa Taifa .
Pia alieleza kusikitishwa na matumizi makubwa ya pesa katika mchakato huu na kuwa anashangazwa kuona wana CCM wakiendelea kuchezea pesa kwa kuandaa mbwembwe nyingi mikoani kwa ajili ya mapokezi yao wakati kila mgombea alipewa taratibu na chama juu ya nini afanye wakati wa kuzunguka kutafuta wadhamini na kuwa pesa zinazotumia zingeweza kusaidia miradi ya kijamii kuliko kuzimwaga kama njugu kwani ni hatari kwa uhai wa chama .















No comments:
Post a Comment