| Kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam Dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA akizungumza wakati wa semina hiyo |
Waumini wa dini pamoja na viongozi mbalmbali na viongozi wa kitaifa katikia nchi zote duniani wametakiwa kuliangalia Taifa la palestina kwa jicho la tatu kutokana na kutengwa na mataifa mengi huku wananchi wa taifa hilo wakiendelea kuteseka kutokana na vita iliyodumu kwa muda mrefu sasa.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania Shekh HEMED JALALA wakati wa semina ya maimam na mashekh kuhusu QUDS (PALESTINA) na matatizo wanayoyapata wananchi wa taifa la palestina na mataifa mengine ya masharaki ya mbali ambayo yamekumbwa na machafuko makubwa kipindi cha karibuni.
![]() |
| Baadhi ya picha za matukio mbalimbali kutoka katimka machafuko huko Palestina |
Amesema kuwa Taifa la palestina ni Taifa ambalo lina mchanganyiko wa dini na madhehebu mbalimbali hivyo wanaoumia katika dhuluma hizo ni watu wa dini zote huku akitanabaisha kuwa kuna haja ya wakristo na waislam nchini na duniani kuungana kwa pamoja kupinga kwa kasi kubwa dhuluma hizo wanazofanyiwa Taifa la palestina.
| Viongozi mbalimbali wa Dini ya kiislam waliohudhuria semina hiyo |
Amesema kuwa Palestina ni nembo ya dunia kwani ndio nchi yenye historia kubwa duniani,na ni alama ya dini zote kwani ina mchanganyiko wa dini mbalimbali,huku akisema kuwa ndani ya taifa la palestina dhuluma yoyote wanayofanyiwa wapelestina ni dhuluma kwa dini zote wakristo pamoja na waislam.
Amesema kuwa kwa sasa wajibu mkubwa wa viongozi wa kidini na wapinga dhuluma kote nchini ni kuhakikisha kuwa wanaueleza ulimwengu juu ya kile ambacho kinatokea katika mataifa hayo likiwemo taifa la palestina,na kuwaeleza watu juu ya umuhimu wa taifa la palestina kwa dunia na historia yake kwa ujumla.
| Nje ya semina hiyo |
Akizumgumzia malengo ya kufanyika kwa semina hiyo kiongozi mkuu wa kiroho wa waislam dhehebu la shea inthnasheriya Tanzania shekh HEMED JALALA amesema kuwa ni kuwakumbusha watanzania kuwa amani hii iliyopo nchini kwa sasa wajue kuwa na taifa la palestina wanahitaji kuwa nayo lakini wanaikosa hivyo watanzania waiangalie palestina kwa jicho la pekee na kuona ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia.

No comments:
Post a Comment