Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, leo kimeendelea na mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa
Benki ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Benki ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Jana kikosi cha Stars kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja wa Taifa wa Ethiopia (Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya Taifa kwa mazoezi.
Taifa Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Misri.
Daktari wa Taifa Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni nzuri kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanya mazoezi katika ukanda wa juu (mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali itakayopelekea wachezaji kuwa fit kwa ajili ya mchezo.
Hali ya hewa ya Alexandria ni ya kawaida, hakuna baridi sana kutokana na kuzungukwa na bahari ya la Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja tutakachokuwa kambini hapa Addis Ababa tunatarajiwa vijana watakua vizuri kabisa kw aajili ya mchezo” Alisema Haonga”.
Wachezaji wote wa Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri, kiafya, kifikra na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao.
Wenyeji Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars kupata mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuelekea nchini Misr
No comments:
Post a Comment