KOCHA mkuu wa Yanga SC, Mholanzi, Hans van der Pluijm anawasili leo usiku jijini Dar es salaam tayari kuanza kazi ya kukinoa kikosi chake kuelekea michuano ya
klabu bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame.
klabu bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame.
Yanga itashiriki kombe la Kagame linalotarajia kuanza Julai 11 mwaka huu sambamba na klabu za Azam fc na Simba.
Bado haijathibitishwa moja kwa moja kama Simba watashikiri Kagame kwasababu wenye haki ni Mbeya City fc walioshika nafasi ya tatu msimu wa 2013/2014, lakini taarifa za kuaminika ni kwamba Mnyama ndiye atacheza mashindano hayo.
Likizo ya Pluijm imemaliza jana na leo anaondoka kwake Ghana na anatarajia kuwasilia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere saa 7:30 usiku.
Hata hivyo, Pluijm amedai habari zinazoripotiwa kwamba ataambatana na wachezaji wawili wa kimataifa ni uongo, lakini kuna wachezaji wakali wa kimataifa watajiunga na Yanga, kinachosubiriwa ni TFF kutoa idadi ya wachezaji wa kimataifa wanaoruhusiwa kusajiliwa.
Yanga na Azam wametuma mapendekezo TFF wakiomba idadi ya wachezaji wa kigeni iongezwe kutoka 5 hadi 8.
No comments:
Post a Comment