What's Trending?

Labels

Ads

Sunday, June 14, 2015

Stars mbichi na mbivu kujulikana leo mbele ya Misri

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) usiku wa leo inakabiliana na Misri katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) itayopigwa kwenye uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria. 
Mechi ya Stars inaanza majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Akiongelea mchezo wa leo kocha wa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru kikosi kimefika salama nchini Misri na kipo katika hali nzuri, vijana wana ari na morali ya hali ya juu, anaamini  timu itafanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya wenyeji Misri.
Nooij amesema mchezo wa leo ni muhimu kwake, na kikosi chake kitacheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, huku safu ya ushambuliaji ikihakikisha inatumia vizuri nafasi itakazozipata.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,  Mh. Juma Nkamia naye yupo jijini Alexandria kwa ajili ya kuipa sapoti Taifa Stars.

No comments:

Post a Comment