Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm tayari ameshawasili jijini Dar es Salaam akitokea nchini Ghana alikokuwa kwa mapumziko mara baada ya kumalizika kwa msimu wa
ligi kuu Tanzania bara 2014-2015 ambapo alikiongoza kikosi cha wanajangwani kutwaa ubingwa wa ligi.Pluijm amerejea kuanza majukumu ya kukinoa kikosi cha Yanga kwa ajili ya michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo ikiwa ni pamoja na mashindano ya Kagane Cup, ligi kuu Tanzania bara na ile ya vilabu bingwa barani Afrika.
No comments:
Post a Comment