Abiria wa ndege moja ya shirika la ndege la Flybe linalohudumu nchini Uingereza walicheleweshwa kwa zaidi ya saa mbili baada ya wahandisi wa ndege hiyo kubaini kuwa nyuki alikuwa amepenyeza na kuingia ndani ya mitambo ya ndege hiyo na hivyo safari haingewezekana.
Ndege hiyo ya Flybe yenye namba ya usajili BE384 iliyokuwa ikitoka Southampton kuelekea Dublin.
Wahandisi walilazimika kutafuta mbinu ya kumtoa mdudu huyo.
Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo Noel Rooney, anasema hakuamini tukio hilo hasa kwani ndge hiyo imeitwa jina la nyuki!
Taarifa kutoka kwa shirika hilo lilisema kuwa nyuki huyo alikuwa ndani ya mitambo muhimu ambayo ingehatarisha maisha ya abiria wake.
''rubani wetu alitahadharishwa na kuwepo kwa nyuki na akalazimika kurejea maramoja katika uwanja wa ndege wa Southampton'.'
Shirika hilo limewaomba radhi abiria wote waliokerwa na hatua ya kurejea kwa ndege hiyo.
Watu wengi waliitania ndege hiyo kufuatia ripoti hiyo kuenea kwenye mitandao ya kijamii.
Rooney aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa ''nimebeba jaa ilikuhakikisha kuwa safari yangu ikamilike''
source BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment