Mchezaji wa Yanga msimu uliopita, Nizar Khalfan, pichani aliyekaa chini na kipa waCoastal Union msimu uliopita, Shaaban Kado, waliojiunga na timu ya
Mwadui ya Shinyanga, leo wamenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Bahi mkoani Dodoma, wakiwa katika usafiri wao binafsi wa gari dogo lenye namba za usajili T444 DCX walipokuwa wakielekea mkoani Shinyanga. Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni kuchomoka kwa tairi la nyuma la gari hilo. Katika ajali hiyo iliyokuwa na jumla ya watu wanne hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya majeruhi, ambapo Kado imeelezwa kuwa ameumia mkono.

Miongoni mwa abiria waliokuwamo katika gari hilo wakizungumza na askari wa usalama barabarani, eneo la tukio.
Gari hilo lililopata ajali likiwa eneo la tukio.

No comments:
Post a Comment