What's Trending?

Labels

Ads

Tuesday, June 9, 2015

NEC kuwaburuza Mahakamani wananchi 100 waliojiandikisha zaidi ya mara moja Daftari la Wapiga kura


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema inakusudia kuwafikisha Mahakamani wananchi zaidi ya 100, wa Mkoa wa Njombe, baada ya kubainika kuwa walijiandikisha zaidi ya
mara moja kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
 
Naibu katibu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Daftari na Tehama, Daktari, Sisi Kariali, amesema kwamba wananchi hao wamebainika kwa kutumia teknolojia inayotumiwa na tume hiyo na kwmaba zoezi hilo litaendelea katika maeneo yote nchini. 
 
Aidha, amesema picha na majina ya watuhumiwa hao yamepelekwa kwenye idara zinazohusika huku akiwaonya wananchi ambao bado hawajaandikishwa kuacha kufikiria kwamba wanaweza kujiandikisha zaidi ya mara moja bila kubainika. 
 
Amesema hadi sasa tume imekamilisha uandikishaji katika mikoa mitano (5), ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa na Njombe na kwamba hadi kufikia Juni 18, 2015, itakuwa imekamilisha uandikishaji kwenye mikoa mingine 8.

Kumekuwepo mjadala mkubwa baada ya kubainika kuwa watu wamekuwa wakijiandikisha zaidi ya mara moja katika vituo tofauti na kuibua hofu ya uchakachuaji mkubwa kufanyika katika Uchaguzi Mkuu 2015

No comments:

Post a Comment