What's Trending?

Labels

Ads

Tuesday, June 9, 2015

Msimamo wa Tegete kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni

hi(1)
SHIRIKISHO la soka Tanzania TFF bado linafikiria kukubali au kukataa ombi la klabu na bodi ya ligi kuhusu kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi kufikia 10.

Klabu tatu kubwa nchini, Yanga, Azam, Simba zimetuma maombi TFF zikitaka kuongezewa idadi ya wachezaji wa kigeni na kinachosubiriwa kwasasa ni maamuzi ya kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka nchini.
Wakati hayo yakiendelea, kocha wa Toto African ya
Mwanza na baba mzazi wa mshambuliaji wa Yanga aliyetimkia Mwadui fc, Jeryson Tegege, mzee John Tegete amepingana na mawazo ya kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni akidai inaua vipaji vya wazawa.
“Sikubaliani na suala la kuongeza wachezaji wa kigeni kwasababu mpira wa Tanzania bado unasuasua na tutazidi kuua viwango vya wachezaji Wazawa. Hata wachezaji watano waliopo sasa wanaua vipaji vya wachezaji wetu. Timu zinawachezesha wachezaji wa kigeni kwasababu zinawalipa fedha nyingi, lakini sio kwamba wana viwango zaidi ya wachezaji wazawa”. Amesema Tegete na kufafanua: “England wanafikiria kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni, sisi ambao hatupo hata kwenye ramani ya mpira tunataka kuongeza”.
“Timu tatu tu ndizo zinaweza kuleta wachezaji 10, vilabu vingine haviwezi, huoni kama hii ni hujuma kwa nchi? Umewahi kuona wapi wachezaji wa timu ya taifa wanachukuliwa kutoka Toto Africa, Mbeya City? wote wanatoka timu tatu tu za Yanga, Simba, Azam na ndio maana timu ya taifa ni mbovu. Hata marisevu wa timu hizo wanaitwa”………..

No comments:

Post a Comment