What's Trending?

Labels

Ads

Sunday, June 21, 2015

Hivi hapa ndivyo vigezo vya wachezaji wa kigeni kuja kucheza Tanzania

Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi ya wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba) wachezaji wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote.
Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:
Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au
Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.
Kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakyocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development Fund).
Pia imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini wataruhusiwa  kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na vilabu vyao

No comments:

Post a Comment