What's Trending?

Labels

Ads

Tuesday, June 16, 2015

AC Milan yamtimua Filippo Inzaghi

filippo-inzaghi-milan_2470kxq4g3jg1k96oeahd7k72
Klabu ya  Ac Milan imethibitisha kumtimua  kocha wake, Filippo Inzaghi baada ya kuwa na msimu mbaya katika ligi ya Serie A na nafasi yake inachukuliwa na Sinisa Mihajlovic.

Mihajlovic ambaye alikuwa kocha wa Sampdoria msimu uliopita, amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho na atalipwa karibia paundi  milioni 2.5 kwa msimu.
Licha ya kumtimua kocha huyo AC Milan wamempongeza kwa kazi yake aliyoifanya akiwa kwenye klabu hiyo.
Ac Milan chini ya Inzaghi  imemaliza msimu uliopita ikiwa imeshika nafasi ya kumi ikijikusanyia  52, wakati Mrithi wake Sinisa alimaliza nafasy ya 7 akiwa na  Sampdoria.

No comments:

Post a Comment