What's Trending?

Labels

Ads

Tuesday, July 26, 2016

Matokeo ya Yanga dhidi ya Medeama yapo Hapa

haya-hapa-matokeo-ya-matokeo-ya-yanga-dhidi-ya -medeama
haya hapa matokeoa ya yanga dhidi ya medeama mechi ya marudiano iliyochezwa leo Jumanne tarehe 26. Yanga imeshindwa kutamba kwa mara nyingine tena kwenye michuano ya kimataifa baada ya kukubali kipigo cha bao 3-1 mbele ya Medeama kwenye mchezo wa Kundi A wa michuano ya kombe la shirikisho Afrika.

Kikosi cha mholanzi Hans van Pluijm kiliruhusu goli la mapema lilifunga dakika ya 7 na Daniel Amoah kabla ya golikipa ya Yanga Deogratius Muish kudaka mkwaju wa penati uliopigwa na nahodha wa Medeama Paul Aidoo kufatia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumwangusha mchezaji wa Medeama kwenye eneo la hatari.

Kabla mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara hawajajipanga vizuri wakapigwa goli lingine la pili, safari hii alikuwa ni Abbas Mohamed aliyepachika bao la hilo baada ya mpira mrefu kumpita mlinzi wa Yanga Kelvin Yondani na kumkuta mshambuliaji huyo ambaye alimfunga Dida kwa ufundi.

Mkwaju wa penati uliopigwa na Simon Msuva uliipa Yanga bao la kwanza na kufanya matokeo kuwa 2-1, penati hiyo ilitokana na Obrey Chirwa kuangushwa kwenye box la hatari la Medeama.

Abbas Mohamed akaifungia Medeama bao la tatu likiwa ni bao la pili kwake kwenye mchezo wa leo ambalo liliimaliza Yanga na kuipa mlima mrefu wa kupanda.

Licha ya Van Pluijm kujaribu kufanya mabadiliko kwa kumtoa Kelvin Yondani na nafasi yake kuchukuliwa na Vicent Andrew ‘Dante’, Haruna Niyonzima akampisha Juma Mahadh na nafasi ya Juma Abdul aliyeumia na kushindwa kuendelea na mchezo ilichukuliwa na Amis Tambwe.

Licha ya Van Pluijm kujaribu kufanya mabadiliko kwa kumtoa Kelvin Yondani na nafasi yake kuchukuliwa na Vicent Andrew ‘Dante’, Haruna Niyonzima akampisha Juma Mahadh na nafasi ya Juma Abdul aliyeumia na kushindwa kuendelea na mchezo ilichukuliwa na Amis Tambwe lakini mabadiko hayo bado hayakubadilisha matoke.

Matokeo hayo yanaendelea kuiacha Yanga mkiani mwa Kundi A ikiwa na pointi yake moja baada ya kucheza mechi nne huku TP Mazembe ambayo itacheza kesho dhidi ya MO Bejaia inaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi 7 ikifuatiwa na MO Bejaia yenye pointi tano baada ya kucheza michezo mitatu. Medeama imefikisha pointi tano pia sawa na Bejaia lakini yenyewe imeshacheza mechi nne mechi moja zaidi ya Bejaia.

No comments:

Post a Comment