What's Trending?

Labels

Ads

Thursday, July 7, 2016

JERRY MURO AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SOKA MWAKA MMOJA


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka.

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza kumfungia Muro kupitia ile kesi yake kwamba amekuwa akiipinga na kuishambulia TFF kwenye vyombo vya habari.

Kikao cha Kamati ya Maadili ya TFF, kilikaa leo bila ya Muro kuwepo kwa kuwa wakati mwaliko unatoka alikuwa nje ya Dar es Salaam.

Awali Muro alisema alikuwa mapumzikoni Machame mkoani Kilimanjaro ambako ni kwao.

No comments:

Post a Comment