Yanga ya Dar-es-salaam imekubali kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Mo Béjaïa ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kuwania Kombe la Shirikisho la Soka Barani Africa-CAF.Goli la kwanza na pekee katika mchezo huo lilipatikana katika dakika ya 20 ya mchezo kupitia kwa Yassin Salh. Hadi mapumziko Yanga walikuwa nyuma kwa bao hilo moja huku wakilazimika kufanya mabadiliko mapema kipindi cha kwanza kuna dakika ya 32 baada ya Oscar Joshua kuumia. Nafasi yake ilichukuliwa na Haji Mwinyi ambaye katika dakika ya 90 alionyeshwa kadi nyekundu kufuatia kuwa alishachukua kadi nyingine ya njano kabla.
Kwa mujibu wa matangazo mbalimbali ya moja kwa moja yakiwemo ya Radio eFM 97 katika mchezo huo kama kawaida mashabiki wa timu za kiarabu walionyesha kila aina ya mbwembwe, zikiwemo tochi kuelekezewa kwa wachezaji hususani kipa wa Yanga.
Hata hivyo Yanga walionekana kucheza kwa uhakika na kujiamini kitu ambacho kinatia matumaini kwamba ushindi unaweza kupatikana katika mechi ya marudiano. Yanga wanarejea Uturuki kuendelea na kambi ili kujiandaa na mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaofanyika tarehe 28/6 jijini Dar-es-salaam.
Katika michezo mingine ya hatua hii ya makundi TP Mazembe ya DRC walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Medeama ya kutoka Ghana. Kawkab Marrakech ya Morocco waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Etoile Sahel ya Tunisia.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment