Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana jumanne alitoa mhadhara wa 13 wa Kumbukumbu ya Rafael M. Salas ulioandaliwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu ( UNFPA), mhadhara huo ulikuwa ni sehemu ya vikao vya mwaka vya Bodi na Mifuko ya Umoja wa Mataifa vinavyoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Pamoja naye Meza Kuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason, Rais wa Bodi, na Balozi Carmelita R. Salas, mjane wa Bw. Rafael M. Salas
Sehemu ya washiriki wa mhadhara wa 13 kumbukumbu ya Rafael M. Salas, uliofanyika siku ya Jumanne ambapo mzungumzaji mkuu alikuwa ni Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete. Tanzania ni Mjumbe wa UNFPA.
Mhe Jakaya Kikwete akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mhadhara wa 13 wa kumbukumbu ya Rafael Salas uliofanyika katika ukumbi wa ECOSOC katika Umoja wa Mataifa.
Dr. Babatunde Osotimehin akielezea jambo kwa Mhe Rais mstaafu Jakaya Kikwete, wengine ni Balozi Carmelita Salas, Mjane wa Rafael M. Salas aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza wa UNFPA.
Na MwandishiMaalum, New York
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema, ingawa idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na uhakika wa maisha yao wala kazi zenye tija na staha wapo katika nchi zinazoendelea, dunia katika ujumla wake inapashwa kuonyesha utashi wa kisiasa na udhubutu wa kuwekeza kupitia vijana.
Amesema, mazingira ya mamilioni ya vijana kukaa
bila shughuli ya aina yoyote kunatoa mwanya kwa
vijana hao kurubuniwa na kutumiwa na watu wasio
kuwa na nia njema na hivyo kutishia hali ya Amani,
usalama na ustawi wa mwanadamu na hatimaye
kushindwa kufikia au kupata faida za kidemograsia
na maendeleo endelevu.
Mhe. Kikwete ameyasema hayo jana(jumanne) hapa
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wakati alipotoa
mhadhara wa 13 wa kumbukumbu ya Rafael M.
Salas. Mhadhara huu ambao mada yake ilikuwa ni “
kuwekeza kwa vijana ili kupata faida ya kidemokrasia
na maendeleo endelevu” uliandaliwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu( UNFPA)
ikiwa ni sehemu ya mikutano ya mwaka ya Bodi za
Mashirika na Mifuko iliyopo chini ya Umoja wa
Mataifa.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria na kushiriki
mhadhara ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson, na Mkurugenzi
Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin , Bi.
Carmelita R. Salas ambaye ni Mjane wa Bw. Rafael
Salas aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza wa
UNFPA, Mabalozi na wataalamu mbalimbali.
“Tafiti na taarifa mbalimbali zikiwamo za Umoja wa
Mataifa, zinaonyesha wazi ongezeko la idadi kubwa
yavijana wanaokadiriwa kufikia 1.8 bilioni idadi ambayo ni hazina na raslimali kubwa, lakini pamoja na uwingi wao, wengi bado wanaishi katika hali ya umaskini uliokidhiri, na ukosefu wa fursa mbalimbali ambazo zingewezesha kuishi maisha yenye staha”.
akasema Kikwete
Na kuongeza kuwa, kati ya vijana hao 1.8 bilioni, 74
milioni hawana ajira akiwaelezea kama vijana
wanaosubiri treni kando ya reli, treni ambayo
haiji.Mazingira haya yanadhihirisha upotevu wa raslimali kubwa ambayo imewekezwa kwa vijana hao na ambao wamepoteza matumaini.
Akafafanua zaidi kwa kutoa takwimu mbalimbali zinazoonyesha tofauti ya faida za kidemokrasia kati ya mabara ya Ulaya, Asia, Amerika ya Latini na Afrika ikiwa ni pamoja na utofauti wa matumizi ya raslimali watu kwa nchi zile ambazo zimethubutu kuwekeza kwa vijana.
Rais Mstaafu Kikwete katika mhadhara wake huo na
ambao ulipokelewa vema sana na wajumbe
waliohudhuria, pia ametoa vielelezo vya kitakwimu
vinavyoainisha namna gani bara la Afrika lilivyo
nyuma karibu katika ikielemewa kila eneo kuanzia
upatikanaji na utoaji wa huduma za uzazi salama,
idadi ya wakunga wenye elimu ya kutosha,
upatikanaji wa huduma za afya, elimu, maendeleo ya kijamii na yenye tija na stahiki na kiwango cha matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango.
“Vijana wakiwezeshwa, wakiaminiwa, wakipewa fursa
na wakithibitishwa wanauwezo mkubwa sana wa
kuleta mabadiliko. Tunatakiwa kuwaamini,
tunatakiwa kuwashirikisha na kuzisikia sauti zao” amesema.
Na kuongeza kuwa , mipango na sera zinazoandaliwa
kwa ajili yao vijana ni vema zikawashirikisha na
kuzingatia mawazo, maoni na matakwa ya vijana.
“
Haya na mengine mengi kwa kutekelezwa kwa
kuzingatia mazingira ya kila nchi na vipaumbele
vyake, tunaweza kugema nguvu kazi hii kubwa
kujiletea maendeleo endelevu pasipo kumwacha
yeyote nyuma” akasisitiza Rais Mstaafu.
Katika hotuba yake hiyo iliyosheheni takwimu na
utafiti wa kisayasi, siyo tu kwamba imeainisha hali
halisi ya mazingira waliyomo vijana bali pia
imechochea majadiliano ya kina.
Baadhi ya mambo ambayo ameyatilia mkazo ni
pamoja na umuhimu wa jamiii kuzingatia usalama na
wa mpango na kuwanadi idadi ndogo ya watoto na
ambayo wazazi wataweza kuimu du na elimu
itakayokidhi mahitaji ya soko la ajira lishe bora na
uchumi imara na endelevu.
Akimkaribisha Rais Mstaafu kuzungumza, Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Elliason
pamoja na mambo mengine alimwelezea Mhe.
Kikwete kuwa ni kiongozi mpenda amani na aliyemstari wa mbele katika kusimamia afya ya mama namtoto.
No comments:
Post a Comment