What's Trending?

Labels

Ads

Saturday, April 9, 2016

TRA YAKAMATA BIDHAA ZA MAGENDO, NI SUKARI NA MAFUTA YA KULA


Na Mwandishi Wetu-Kilwa
Siku ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha (FAST) wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara aitwaye
Yusuf Barkat Sareh, Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu. Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo.
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko762 Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135
Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49 Betri aina ya tigger katoni 223 Amira katoni 135
Sabuni za kufulia katoni 48 Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari.
Mashine mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini nya sukari vya Kilombero,TPC na Mtibwa Sugar. Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India 2000 Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari36,000 mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo25 kiasi cha 1150 Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609 Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.


sehemu ya kuweka sukari na kupima.

Nyumba inayotumika kuweka sukari

Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayomboakionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.

Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.

Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba

Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango


Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.

Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akionesha sukari.

Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania      
                            
Aina ya mafuta kutoka nje ya nchi tayari kuwekwa kwenye ndoo kwa kupeleka Sokoni

Polisi akilinda viroba vyenye sukari kutoka nje ya nchi.

Madumu yaliyokua na mafuta ya kula na ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta

Nyumba ya mtuhumiwa Yusuf Sareh iliyopo Somanga Njia nne Kikanda. Nyumba hii ndiyo Ofisi ya Bosi ambayo utumika kuweka bidhaa kabla ya kusambazwa sokoni iliyopo Somanga njia nne eneo la Kikanda Wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.
………………………………………………………………………………………………
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                                                                    

No comments:

Post a Comment