What's Trending?

Labels

Ads

Thursday, March 10, 2016

Liverpool yaiadhibu Manchester United 2-0 Europa League.

Liverpool wameanza vyema kampeni zao kwenye michuano ya Europa League hatua ya 16 bora baada ya kuiangushia kipigo Manchester United cha bao 2-0 kwenye uwanja wa Anfeild jana usiku.
Kikosi cha Jurgen Klopp kilitawala mchezo huo kwa asilimia kubwa ya mchezo huo wa kwanza kati ya timu hizo za Premier League giants huku kocha huyo wa kijerumani akifurahia ushindi wake dhidi ya United.
Daniel Sturridge aliipa Liverpool goli la kuongoza dakika ya 15 kwa mkwaju wa penati baada ya Memphis Depay kumfanyia madhambi Nathaniel Clyne kwenye eneo la hatari penati ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wadau wakikosoa kwamba ilikuwa ni nje ya penalty box.
Roberto Firmino akaongeza bao jingine kwa shuti kali la karibu zikiwa zimesalia dakika 17 pekee mchezo huo kumalizika.
United haikutengeneza hata nafasi moja ya kufunga, ubora wa golikipa wao David de Gea ndiyo umeikoa United kuchezea idadi kubwa ya magoli kwenye mchezo huo baada ya mlinda mlango huyo wa Hispania kuokoa michomo mingi.
Rekodi zilizowekwa kwenye mchezo huo:
Manchester United hawajashinda mchezo wowote wa ugenini kati ya michezo yao sita iliyopita kwenye hatua ya moano ya michuano ya Ulaya, wamepoteza michezo mitano kati ya hiyo.
United imepata clean sheet moja kwenye mechi 10 walizocheza kwenye uwanja wa Anfield kwenye mechi za mashindano yote.
Daniel Sturridge amefunga magoli matano na ku-assist goli moja kwenye mechi saba dhidi ya United kwenye mashindano yote.
United wamepigiwa mashuti nane on target dhidi ya Liverpool, mashuti mengi zaidi kuziuwa na klabu hiyo ndani ya mechi moja msimu huu.
Roberto Firmino amefunga magoli matatu mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye mechi za Liverpool. 
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                                                                    

No comments:

Post a Comment