Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika hapo leo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuelekea Ikulu jijini Dar es salaam kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.
Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi Simon Siro amesema Chama hicho kinatakiwa kutumia mbinu nyigine ya kushinikiza kurejeshwa kwa matangazo hayo ya Televisheni ya Taifa na sio kupitia maandano.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment