Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Masasi Mkoani Mtwara FORTUNATUS KAGORO amemtangaza rasmi CHUACHUA RASHID wa CCM kuwa mbunge baada ya kupata kura kupata kura 16597 dhidi ya mpinzani wake wa karibu ISMAIL MAKOMBE maarufu kama KUNDAMBANDA wa CUF aliyepata kura 14069 KATIKA Uchaguzi mdogo uliofanyika Kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Masasi Ajali Mussa amesema mikakati na sera za chama chake ndiyo ilikuwa siraha ya ushindi wao Huku mshindi wa ubunge Chuachua Rashid akisema ilani ya CCM iligusa maslahi ya wananchi ndiyo maana wamewaamini kuwachagua.Desemba 20 kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge jimbo hilo Dk Emmanueli Makaidi wa NLD Wakala wa majumuisho wa CUF Maftaha Nachumba ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtwara mjini amekubali matokeo na kusema kuwa tofauti iliyojitokeza ni ndogo lakini kilichowaangusha zaidi ni mwitikio mdogo wa wananchi waliojitokeza kupiga kura.
MATOKEO:
1.RASHID CHUACHUA-CCM KURA 16567
2.ISMAIL MAKOMBE(KUNDAMBANDA) CUF KURA 14069
3.MUSTAPHA SWALEHE-CHADEMA KURA 512
4.DK.PETER TIMOTHY MROPE-ACT WAZALENDO KURA 347
5.ANGELUS THOMASI-NLD KURA 70
MATOKEO:
1.RASHID CHUACHUA-CCM KURA 16567
2.ISMAIL MAKOMBE(KUNDAMBANDA) CUF KURA 14069
3.MUSTAPHA SWALEHE-CHADEMA KURA 512
4.DK.PETER TIMOTHY MROPE-ACT WAZALENDO KURA 347
5.ANGELUS THOMASI-NLD KURA 70
No comments:
Post a Comment