What's Trending?

Labels

Ads

Wednesday, November 18, 2015

kAFULILA ATIMBA MAHAKAMA KUU KUPINGA USHINDI WA CCM..HUKU AKIWA NA MATOKEO YOTE YA UCHAGUZI.

Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR -Mageuzi, David Kafulila, amewasilisha pingamizi katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, kupinga ushindi wa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasna Mwilima.
Akizungumza jana baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Kafulila alisema amefungua kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015 ya uchaguzi, akiwalalamikia Mwilima, msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa serikali.
Alisema kesi hiyo itasimamiwa na mawakili wawili, Tundu Lissu na Daniel Lumengela, huku hoja ya msingi katika shauri ikiwa ni kupinga matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi ambayo anadai si halali kwani kutokana na fomu 382 za vituoni na kusainiwa na wasimamizi na mawakala, alipata kura zaidi ya 34,000 dhidi ya 32,000 za mpinzani wake (Mwilima).
                                    
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        


No comments:

Post a Comment