Mgombea ubunge katika Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa na watu wengine watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa leo na kusomewa mashtaka manne, ikiwemo la
uvunjivu wa amani.
uvunjivu wa amani.
Hata hivyo, wengine sita hawakuweza kufika mahakamani hapo leo lakini mahakama hiyo imeelezwa kuwa washitakiwa hao wataunganishwa katika kesi hiyo.
Mbali na uvunjifu wa amani, mwanasiasa huyo machachari na wenzake wanakabiliwa na makosa mengine yakiwemo kuharibu mali na kujeruhi polisi.
Hata hivyo, Msigwa na wenzake wameyakana mashtaka yote waliyosomewa leo na kuachiwa baada ya kukidhi vigezo vyote vya kupewa dhamana. Kesi yao itatajwa tena Novemba 2, mwaka huu.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, Mchungaji Msigwa alikuwa ni miongoni mwa wafuasi 64 wa Chadema walitiwa mbaroni na kulala rumande usiku mmoja.
No comments:
Post a Comment