What's Trending?

Labels

Ads

Tuesday, October 6, 2015

Magufuli akiri udhaifu huu wa serikali kwa wananchi

Mgombea urais wa chama cha mapinduzi CCM , Dk. John Pombe Magufuli, amefichua siri nzito ya chuki ya wananchi kwa serikali yao kuwa ni vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wake na vigogo wa serikali.
Kwa vile anajua sababu za chuki za wananchi kwa serikali yao amewaomba wampigia kura nyingi za ndiyo Octoba 25 ili awachukulie hatua na kukomesha hali hiyo.

Alisema hayo jana katika kampeni zake huko Hanang, mkoa wa Manyara na kufafanua kuwa yeye ni tingatinga hivyo wakimchagua atasafisha mafisadi na wabadhirifu wote serikalini.
Aliongeza kuwa, kamwe hatakuwa na msamaha dhidi ya mafisadi na wala rushwa kwani mara zote wamekuwa wanakwamisha huduma za jamii zinazotelewa na serikali hivyo kusababisha wananchi kuchukia serikali.

Alisema Watanzania wamechoshwa na maisha duni hivyo wanahitaji rais ambaye atasimamia rasirimali zao  na mabadiliko ya kweli ambayo anaamini yataletwa na rais kutoka CCM. “Niombeeni niingie ikulu nisiwe na kiburi…nataka niwatumikie Watanzania wote bila kujali vyama vyenu, maana mmeteseka sana na shida zilizosababishwa na mafisadi.Vitu vimepanda bei kwa sababu ya ufisadi, Nataka kukomesha yote hayo," alisema

No comments:

Post a Comment