What's Trending?

Labels

Ads

Tuesday, June 9, 2015

TAZAMA VIDEO MPYA YA ALI KIBA ALIYOFANYA NA DIRECTOR WA TANGAZO LA BEATS..




Msanii Alikiba alikuwa nchini Afrika Kusini akifanya video yake mpya anayotarajia kuitoa hivi karibuni na director, Meji Alabi mwenye makazi yake katika mji wa London huko England...

Kwa siku kadhaa Alikiba amekuwa akipost picha na Director Meji ambae ameishi nchini Marekani kwa muda mrefu na kuwa na uzoefu wa kushoot video za kampuni kubwa kama Beats by Dre na video tofauti za wasanii pamoja na filamu. 

Je wajua Director Meji ndio alifanya video ya Beats By Dre x Berlin x Axwell
Mjue kwa Undani Director Meji ...
Kupitia Tovuti ya Director Meji iitwayo  'http://mejialabi.com  
ameandika wasifu wake na pia kuorodhesha kazi ambazo
ameshawahi kuzifanya ikiwemo Tangazo la Beats by Dre x Berlin x Axwell.
Video hio ya kampuni ya Beats ilifanyika huko Berlin mwaka 2013 katika sherehe ya 
kuzindua Studio mpya za beats. Sherehe hio ilihudhuriwa na dj's tofauti 
pamoja na Rapa maarufu nchini Uingereza Tinie Tempah na Giggs

Meji akiangalia kwa makini wakati wakushoot video.
Meji  amekuzwa nchini Marekani ila kwasasa makazi yake yapo katika mji wa London huko England. 
Meji pia amefanya kazi za aina tofuati kuanzia za muziki mpaka documentaries.

Alikiba na Abdul Kiba wakielekea Washington Dc kufanya Show
                  Kazi yake ya hivi karibuni aliofanya Meji ni video ya Asa - Eyo (Click kuangalia video hio) pia unaweza kuangalia video ya Beats-By-Dre-x-Berlin-x-Axwell iliofanywa na Meji.
katika Wasifu wake Meji aliandika anapenda kutengeneza Filamu pia.

No comments:

Post a Comment