Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo na muhtasari wa ziara yake toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson Masilingi baada ya kuwasili The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya Shell Bw. Ben van Beurden jijini the Hague, Uholanzi leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Bert Koenders jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katikati wakati Waziri wa Zanzibar Mhe Ramadhani akigonganisha glasi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Mark Rutte jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson Masilingi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mfalme Willem Alexander katika kasri la Kifalme la Noordeinde jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kuongea na Mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Uholanzi jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mhe Mark Rutte jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015. PICHA NA IKULU
Jeshi la Polisi mkoani Iringa limekamata mikanda ya DVD yenye mafunzo ya kijeshi yanayohusiana na kikundi cha ugaidi cha Al Shaabab cha nchini Somalia zilizokuwa zikitumika na watoto wa mitaani wanaodaiwa kuwa walikuwa wakichukua mafunzo kwakutumia DVD hizo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP.Ramadhan Mungi ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari akieleza kuwa mikanda hiyo ilikuwa ikitumiwa na vijana hao wanne wenye umri kati ya miaka 12 na 16 inaonesha ukatili na mauaji yanayodaiwa kufanywa na kikundi cha kigaidi cha Al Shaabab mikanda ambayo walikuwa wakiitazama kwa kutumia kompyuta mpakato yaani laptop. Aidha kamada Mungi amesema pamoja na mikanda hiyo ya DVD pia jeshi hilo limekamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya bangi wakiwa na magunia matatu ya bangi katika harakati za kufunga bangi hiyo kwenye vifurushi vidogo tayari kuisambaza kwa wateja wao. Mungi ameongeza kamata hiyo iliyofanywa na jeshi hilo mkoa wa Iringa pia imekamata nguzo 35 za umeme za shirika la umeme nchini Tanesco nyaya za kusambaza umeme na vifaa vingine zikiwa zimehifadhiwa kwa watu binafsi wawili ambao hakuwataja majina kwa sababu za kiupelelezi.
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ
No comments:
Post a Comment