Timu ya Mbeya City Fc, leo imefanya Kliniki maalumu ya soka kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 8-15 kwenye uwanja wa FFU jijini Mbeya.
Kliniki hiyo yenye lengo la kusaka vipaji ambavyo vitaingizwa moja kwa moja kwenye timu za vijana za City
chini ya umri huo, imefanyika chini ya usimamizi wa makocha Mohamed Kijuso na Rashid Kasiga.
chini ya umri huo, imefanyika chini ya usimamizi wa makocha Mohamed Kijuso na Rashid Kasiga.
Mara baada ya kliniki hiyo kukamilika, kocha Kijuso ameuambia mtandao huu kuwa amefurahishwa na mwitikio wa vijana waliojitokeza kuja kupata mafunzo ya soka huku akisifia vipaji vingi alivyoviona siku ya leo kutoa kwa vijana hao wadogo.
“Nimefurahishwa na mwitikio wao, hii inaonyesha kuwa vijana wengi wanataka kucheza mpira na wanaupenda, kuna vipaji vingi nimeviona, kwa kuwa hii jambo ni endelevu nina uhakika tutaibua vipaji vingi ambavyo vitakuwa manufaa kwa City na timu ya Taifa hapo baadaye” alisema Kijuso.
Akiendelea zaidi Kijuso alisema kuwa anafahamu lengo la uongozi wa Mccfc kuanzisha kliniki hii hivyo basi kila rekodi itanayomuhusu kijana atakayepita kwenye mafunzo haya itatunzwa vizuri.
“Watoto leo wamejitokeza wengi, ndiyo maana tuliwagawa kwenye makundi matatu, imani yangu wikiendi ijayo watakuwa wengi zaidi, ni vizuri kutunza kumbukumbu ya kila mmoja kwa ajili ya kile kilichopangwa kufanyika baadaye, lengo la uongozi ni kuwa na timu imara za vijana, nafahamu hilo na niko makini kwenye kuweka kumbukumbu hizi” alisema Kijuso huku akimalizia kuandika jina la mmoja wa watoto waliokuwepo uwanjani.
No comments:
Post a Comment